
Rai hiyo ameitoa katika hafla ya utekelezaji wa Ilani hiyo
iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Donge, Nd. Sadifa Juma katika jimbo
hilo huko Kaskazini “B” Unguja.
Dkt. Mabodi aliwambia viongozi wa kisiasa waliochaguliwa na wananchi
kuanzia ngazi za Madiwani, Wawakilishi, Wabunge na Rais wa Zanzibar
kuwa utaratibu wa kubuni na kutekeleza miradi ya maendeleo sambamba na
kuimarisha miradi ya huduma za kijamii sio suala la hiari bali ni lazima
kwa kila aliyetumia tiketi ya chama hicho kuomba ridhaa ya kuwatumikia
wananchi.
Naibu Katibu Mkuu huyo amesifu juhudi za baadhi ya viongozi
wanaoendelea kutekeleza ahadi walizoahidi kwa wananchi awamu kwa awamu
kuanzia ngazi za chini hadi taifa, na kuwataka waliojisahau kurudi
Majimboni mwao kutatua kero zinazowakabili wananchi.
“ Njia pekee ya CCM kubaki madarakani ni kutatua kero za wananchi
mijini na vijijini bila kujali itikadi za kisiasa na kidini ili jamii
endelee kujenga imani na upendo wa kudumu kwa Chama kilichoiweka
serikali madarakani”, alisema Dkt. Mabodi.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt. Mabodi alitoa ahadi ya
shilingi 300,000 kwa skuli ya maandalizi Mkataleni pamoja na kusaidia
ujenzi wa vyoo vya skuli hiyo ili watoto waweze kusoma katika mazingira
bora.
Akizungumza Mbunge wa Jimbo hilo, Nd. Sadifa Juma mara baada ya
kutoa mabati 400 yenye thamani ya shilingi milioni saba ili kuezekea
Hospitali ya Vijibweni, Maskani ya Kitaruni, Maskani ya Karange,
vijibweni “B” Maskani, Donge bridge, pamoja na Skuli ya maandalizi ya
Mkataleni.
Aidha Nd.Sadifa mbali na kugawa mabati hayo pia alitoa fedha taslimu
zaidi ya shilingi milioni 1.5 kwa hospitali ya Vijibweni inayotegemewa
na wananchi wa Jimbo hilo na maeneo jirani kwa huduma mbali mbali za
afya ili kiweze kufanyiwa matengenezo na kuwa cha kisasa.
Akitoa shukrani zake Daktari dhamana wa Kituo hicho, Bi.Miza Ali Ussi
alipongeza juhudi za mbunge huyo na alisema msaada huo umepatikana kwa
wakati mwafaka kwani kwa muda mrefu walikuwa wakikabiliwa na changamoto
za upungufu wa vifaa tiba na mabati ya kuezekea baadhi ya nyumba za
hospitali hiyo.
chanzo: zanzibar24.
Comments