Aliyenusurika kufa Kibonde Mzungu aelea tukio lilivyotokea.

Kufuatia tukio lilitokea hapo jana maeneo ya fuono kibonde mzungu la mtu mmoja kufariki dunia na mwengine kuokolewa na kufikishwa katika hospitali ya mmnazi mmoja, Majeruhi wa tukio hilo anaeleza uhalisia wa tukio lilivotokea.

Mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Paulo anaeleza:-

” wakati napita maeneo ya Kibonde mzungu na pikipiki yangu kufika sehemu nilihisi maji yananivuta sana ndipo nikaamua kuchupa kutoka kwenye pikipiki na kaanza kuogelea huku maji yakinivuta,
mara nikaona kuna gari yaChuo kikuu imesimama na nikaona watu wengi wakishuka ndani ya gari ile, mmoja kati ya watu walioshuka nikamuona anakuja kwa lengo la kuniokokoa,aliingia kwenye maji akaanza kuniambia “sogea kwa hapa nilipo” nikwamwambia siwezi, ghafla nikamuona kazama chini na sikumuona kuja juu tena”

“Maji yakaendelea kunivuta mpaka kufika maeneo ya katikati ambapo  pana mti ndio nikaukamata ule mti mpaka nilipokuja kuokolwewa”
Chanzo: zanzibar24.

Comments