
Imedaiwa mahakamani hapo na muendesha mashtaka Suleiman Maulid mbele ya hakimu Isaya Kayange kuwa mtuhumiwa huyo amedaiwa kufanya kosa hilo tarehe 17/6 2015 huko Kiembe samaki Mkoa wa mjini magharib Unguja ambapo alimuua Samira Sultani Abdallah jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mtuhumiwa hakutakliwa kujibu lolote na amepelekwa rumande hadi tarehe 1/6 mwaka huu kesi ya ke itakapotajwa tena.
Itakumbukwa kuwa mifupa ya marehemu huyo ilikuywa ndani ya shimo la karo na wazamia lulu mwezi machi mwaka huu.
chanzo:zanzibar24.
Comments