Mtuhumiwa huyo alimkata Mackrina mikono yote miwili hadi kukatika
kabisa na kusababisha kifo chake. Akisomewa hukumu hiyo katika kesi ya
mauaji Mahakama Kuu yenye namba 181/2 /2017, Mei 5, mwaka huu katika
kikao cha Mahakama Kuu kinachoendelea katika Mahakama wilayani ya Tarime
mkoani Mara Jaji wa Mahakama Kuu ya Kanda ya Mwanza, Joaquine De- Mello
alidai kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka
ukiongozwa na mwanasheria wa serikali, Harry Mbogoro.
Mwanasheria huyo wa serikali alidai kuwa mtuhumiwa Chacha Magige
alitenda kosa hilo Julai 2, mwaka 2011 asubuhi katika Kijiji cha Mrito
kwa kumshambulia kwa kumkatakata kwa panga Mackrina, mikono yote miwili
na kukatika, alimshambulia kichwani na kumsababisha kifo, baada ya
kumnyang’anya mwanamke huyo simu yake ya mkononi na Sh 1,000,000.
Katika mashitaka hayo mtuhumiwa alikiri kumuua mwanamke huyo na kudai
kuwa ilikuwa ni hasira za kumdai shilingi 10,000,000 alizodai alimpa
amhifadhie na kwamba walikuwa na mahusiano ya karibu na Mackrian na
kuiomba mahakama hiyo kumuadhibu kwa kuua bila kukusudia.
Hata hivyo, Mwanasheria wa Serikali Mbogoro alipinga utetezi huo na
kudai kuwa mtuhumiwa alikuwa na nia ya kuua kwani Mackrina alikutwa na
majeraha manne makubwa ya kukatwa mikono yote miwili, jeraha kubwa
ubavuni na kichwani.
Jaji Joaquine akitoa hukumu alikubaliana na maelezo ya mwanasheria wa
serikali na kumtia hatiani kwa kosa la kuua kwa kukusudia. Mtuhumiwa
baada ya hukumu hiyo aliomba maji ya kunywa.
chanzo:habarileo.
Comments