Watu 8 waliozama na boti ya uvuvi jana wapatikana wakiwa hai.

boti
Wavuvi 8 ambao jana hawakupatikana baada ya boti yao ya uvuvi kuzama maeneo ya magharibi ya kisiwa cha tumbatu tayari wameshapatika wakiwa wazima na kufikiswa katika hospitali Kivunge huku hali zao  zikiwa zinaendele vizuri.

Watu hao wameokolewa na wavuvi  katika maeneo ya nungwi wakiwa wanaelea katika ubao waliofunga na madumu ili kuweza kijinusuru.

Boti hiyo  ya uvuvi iliyozama jana inajulikanwa kwa jina la SHOO ambayo ina milikiwa na Omar Kombo mwenyeji wa Kojani ilizama katika maeneo ya magharibi ya kisiwa cha tumbatu baada ya kukubwa na dharuba ya upepo wakati ikiwa katika shuhuli zake za uvuvi.
Boti hiyo iliyokua imebeba watu 50,  watu 42 waliokolewa jana na wengine 8 tayar wameshaokolewa leo uko maeneo ya  Nungwi wakiwa hai.
chanzo:zanzibar24.

Comments