
Akizungumza na Zanzibar24 huko ofisini kwake Mwanakwerekwe Afisa Afya
Kitengo cha Malaria Khamis Ameir Haji amesema kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha bado hakuna mabadiliko makubwa juu ya maambukizi
ya Malaria hivyo jamii inapaswa kuwa na tahadhari ya kina kwa kuimarisha
usafi wa mazingira kwa kufukia vidimbwi vya maji machafu na kulima
vichaka katika maeneo yao.
Aidha ameyataja maeneo yanayoongoza kuwa na wagonjwa wa malaria
Pujini, Majenzi, Kengeja Kisiwani Pemba na kwa upande wa Unguja ni
Uzini, Miwani, Donge kipange, Kilimahewa bondeni, Karakana,Kwaalinatu na
miembeni.
Ugonjwa wa malaria umepungua hapa Zanzibar chini ya asilimia moja
kutokana na utafiti uliofanywa tokea mwaka 2004 hadi 2006 ukilinganisha
na miaka iliyopita ugonjwa huo ulikuwa asilimia 30 hadi 40 .
chanzo:Zanzibar24.
Comments