wakuu wa idara za smz washauriwa kutoa mashirikiano na waandishi wa habari Pemba .



Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh Mwanajuma Majid Abdallah amewataka wakuu wa taasisi za serekali kutoa mashirikiano yao yadhati kwa waandishi wa habari kwa kuwapatia taarifa ili kuwawezesha wananchi kufaham juhudi zinazochukuliwa na serekali katika kuwaletetea maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maadhisho ya siku ya malaria dunia yalio fanyika katika ukumbi  wa  Uwanja wa mpira Gombani Stadiam Chake Chake Pemba amesema ni haki yakila  kiongozi kutoa   habari juu ya kile kinacho fanyika  ili wananchi waondokane na dhana yakua serekali waifanyii chochote cha kuwaletea maendeleo ndani ya maeneo yao.


Amefahamisha kuwa endapo wakuu hao  hawatotoa taarifa kutapelekea kudumaza sekta za serekali nahatimae kushindwa kutekeleza malengo waliyo yakusudia.

Amesema wakati umefika kwa viongozi kubalika na kutoa taarifa pale panapo stahiki ili kujenga imani kwa wananchi juu ya serekali yao.

Katika maadhimisho haya Bi Mwanajuma amewakumbusha wananchi kuvitumia vyandarua vinavyotolewa na serekali kwa malengo yaliyo kusudiwa ikiwa ni pamoja nakujikinga na maradhi ya  malaria yanayo onekana  kuwathiri zaidi akina mama na watoto na sio vinginevyo.

Aidha amesema kuwa katika kupambana na maradhi hayo jumla ya vyandarua 28689 vimegawanywa ndani ya wilaya zote za pemba kwa mwaka 2016 ikiwa na lengo la kuwakinga wananchi na ugonjwa huwo.

Sambamba nahayo ameeleza kuwa licha ya kutolewa kwa vyandaruwa hivyo serekali imeandaa mkakati wakupiga dawa majumbani ili kumaliza kabisa ugonjwa huwo amabao umeonekana kufanikiwa kwa aslimia 99 hapa nchi.

Akichangia katika mkuna huo mmoja kati ya waandishi hao Hajji Nassor amesama watashindwa kutoa taarifa kwa wananchi juu ya mambo mbali mbali yanayofanywa na taasisi hizo kutokana na baadhi ya wizara kutotoa mashirikiano kwa waandishi wa habari ikiwemo Wiazara ya Afya na Wizara ya Elimu.

Nae Bakar Mussa kutoka gazeti la zanzibarleo amewaasi wakuu wa taasisi za serekali kuto waona waandishi wa habari  maadui nabadala yake kuungana kwa pamoja ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Comments