
Akizungumza katika ufunguzi wa Semina ya siku moja kwa vyombo vya habari huko katika ofisi ya Mamlaka ya kuzuiya rushwa Viktoria garden Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,
Utumishi wa Umma na Utawala bora Khamis Juma Maalimu amesema waandishi wa habari wananafasi kubwa katika mapambano dhidi ya rushwa hivyo ili kuleta mabadiliko nivyema kuwa mstari wambele katika kushirikiana na serikali kudhibiti tatizo hilo nawaitumie vyema kalamu zao.
Hata hivyo amesema tatizo la rushwa limekuwa kero kubwa kwa wananchi hasa wanyonge na inapelekea kudumaza maendeleo ya nchi hivyo ili kuunga mkono jitihada za serikali ni wajibu wa watu kupambana na kuwafichua wanaotenda vitendo hivyo viovu kwani kuna baadhi ya watu hutumia madaraka yao vibaya na kutopatikana kwa haki za msingi kwa wananchi.
Kwaupande wao waandishi walioshiriki semina hiyo wamesema ili kushirikiana katika kupambana na vita hivyo nivyema serikali inaweka mazingira bora kwa utendaji kazi kwa waandishi ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi ili kushinda vita hivyo hapa nchini.
Akifunga semina hivyo Naibu katibu Mkuu wa Wizara Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria na utumishi wa umma Kubingwa Mashaka Simba ametoa wito kwa waandishi wa habari kuzidisha bidii katika mapambano hayo kwani bila ya ushirikiano wao serikali haitaweza kupiga hatua katika kudhibiti tatizo hilo.
Semina hiyo ya siku moja kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Mamlaka ya kuzuiya rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar ikiwa na lengo la kuwaelimisha waandishi kuripoti matukio ili kuwafikisha katika vyombo vya sheria watenda vitendo viovu.
chanzo: Zanzibar24
Comments