Serikali imeahidi kuwa italirejeshea Shirika la Posta Tanzania kiasi cha shilingi bilioni 3.2 ambazo ilizitumia kuwalipa wastaafu wa lililokuwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki ifikapo kufikia 30 Juni mwaka huu itakuwa imelipa kiasi cha Sh3.2bilioni zinazodaiwa na Shirika la Posta Tanzania.
Ahadi hiyo imetolewa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na MIpango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ludewa, Deo Ngalawa (CCM), aliyehoji Serikali ilikuwa na mpango gani wa kuwalipa wastaafu hao yenyewe moja kwa moja bila ya kutumia fedha za mfuko wa Shirika hilo.
‘’Shirika linasuasua kujiendesha, fedha ambazo zilikuwa zitumike kwenye operation ndizo hizo zimekuwa zikitumika kuwalipa Wastaafu wa Afrika Mashariki ili kulinusuru Shirika hilo serikali haioni umuhimu wa kulipa deni hilo.” alihoji Ngalawa.
Comments