Sera ya nishati na gesi kunufaisha Watanzania.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani SERA mpya ya nishati na ya gesi zinalenga kutoa fursa ya raslimali ya gesi asilia kuwanufanisha Watanzania wote wakiwamo waliomo katika eneo inapopatikana raslimali hiyo.

Sera ya nishati ni ya mwaka 2015 na ya gesi ni ya mwaka 2013.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani alibainishwa malengo ya sera hizo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Abdallah Nachuma (CUF).


Mbunge Nachuma alimuuliza Naibu Waziri ni lini serikali itasitisha usafirishaji wa gesi kutoka mtwara kwenda Kinyerezi ili wana Mtwara wanufaike na ajira zinazotokana na uchakataji wa gesi hiyo.

Dk Kalemani alisema, kuna miradi miwili inayosafirisha gesi asilia kutoka Mtwara na Lindi hadi Dar es Salaam, miradi hiyo mipya, mmoja ulikamilika mwaka 2015 na wa Songas ulikamilika mwaka 2004.

Alisema, gesi inayochakatwa Madimba, Mtwara inasafirishwa kwa bomba kwenda maeneo mbalimbali nchini kwa matumizi mbalimbali yakiwamo ya Mtwara, Lindi, Mkuranga na Dar es Salaam.

Dk Kalemani alisema,visima viwili vya gesi katika eneo la Mnazi Bay vimetengwa rasmi kwa ajili ya kupeleka gesi katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Pamoja na gesi asilia kutoka mikoa hiyo kutumika kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji takribani asilimia 50 ya umeme unaotumika nchini, gesi hiyo pia inatumika katika miradi ya kusambaza gesi nyumbani na viwandani katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.

Dk Kalemani alisema, Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini inatekeleza mradi wa kuunganisha gesi hiyo katika Kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara utakaohitaji takribani futi za ujazo milioni 45.

Pia alisema shirika hilo liko kwenye majadiliano na kiwanda cha Urenex kinachotarajiwa kujengwa mkoani Lindi ili kiweze kuunganisha gesi
chanzo:Habarileo.

Comments