Rais azindua mabweni ya UDSM.

Rais John  Magufuli amezindua rasmi mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo.
Rais amezindua mabweni hayo huku akiusifu Wakala wa Majengo(TBA) kwa kumaliza kuyajenga mabweni hayo kwa wakati na kwa uaminifu.
Pia alilisifu Jeshi la Wananchi wa Tanzania na Jeshi la Kujenga Taifa, kwa kujenga mabweni hayo kwa uzalendo, kwa wakati na kwa bei nafuu.
Kadhalika aliisifu  Wizara ya Elimu kwa kukubali kuwatumia wakandarasi wa ndani akieleza kuwa huo ndiyo uzalendo wa kweli.
chanzo:Mwananchi.

Comments