
Kufuatia tukio hilo leo Aprili 24, 2017 Wakurugenzi wa kitaifa na
Wajumbe wa Baraza Kuu wa CUF chini ya Julius Mtatiro imeenda Kituo cha
Polisi cha Kati kukutana na Kamishna Simon Sirro.
kupitia ukurasa wa instagram wa Julius Mtatiro ameandika kuwa “Kamishna Sirro ana roho ya kipekee sana ni Ofisa wa Polisi wa mfano, ametupokea na ametupatia ushirikiano mkubwa sana.” na kujadili mambo kadha wakadha kama ifuatavyo:-
1. Tumempa barua rasmi na ushahidi wa matukio yote ya jinai ambayo chama kimetendewa tangu Agosti mwaka 2016 huku wafanya matukio hayo mabaya wakilindwa.
2. Tumezungumza kwa kina juu ya tukio la Uvamizi wa Vina Hotel na kutaka hatua zichukuliwe haraka.
3. Kamishna Sirro amesikitishwa sana kusikia kuwa viongozi wa chama wameitwa Magomeni ili wapatanishwe na wavamizi/majambazi/mungiki/mazombi. Sirro amekataa utaratibu huo na anasema kuwa makosa ya jinai hupelekwa mahakamani, hayasuluhishwi na Polisi.
4. Tumemkumbushia Kamishna matukio 13 ya jinai ambayo yametendwa na Lipumba na genge lake dhidi ya chama yakiwemo kuteka, kupiga, kuchoma visu, kuvamia n.k. tumemwambia kuwa katika matukio yote hayo, Lipumba na genge lake wameendelea kulindwa.
5. Tumemweleza Kamishna kuwa sisi tumeendelea kuwataka wanachama wawe
watulivu ili tuone hatua za POLISI na kwamba hatua zisipochukuliwa,
sisi tutachukua hatua.
6. Tumemkumbusha Kamishna Sirro kuwa sisi (chama) ni wengi kuliko
Lipumba na Genge lake na kwamba wingi wetu ni silaha kubwa sana na
kwamba tunao uwezo wa kuwasambaratisha mara 100 ikiwa tunataka. Lakini
sisi bado ni wastahimilivu, tunataka kuona hatua zinachukuliwa na POLISI
7. Kamishna Sirro ameahidi kuwa anachukua hatua, ameelekeza mapungufu
yetu, amekubali baadhi ya mapungufu yao na kutoa maelezo baadhi ya
mambo muhimu. Hatuwezi kumhukumu Sirro kwa sasa, ila tutamhukumu
tukishaona hakuna hatua zinazochukuliwa.
chanzo:zanzibar24.
Comments