Alitoa kauli hiyo mara baada ya kushiriki hitma na kuzuru kaburi la
Sheikh Karume lililoko Afisi Kuu za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui
mjini Unguja wakati wa maadhimisho ya kifo cha Rais wa kwanza wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Shehe Abeid Karume
sambamba na siku ya mashujaa Zanzibar.
Alisema ni muhimu kwa wananchi kutenga muda wao na kuwaombea viongozi
wetu waliotangulia mbele ya haki, lengo likiwa ni kukumbuka na kuenzi
mchango mkubwa waliotoa katika kujenga msingi wa maendeleo ya taifa.
Waziri Mkuu alisema Watanzania wote Bara na Visiwani ni wamoja
kiasili, hivyo wanapaswa kushirikiana katika kudumisha misingi
iliyoachwa na waasisi wa taifa ili kuweza kujiletea maendeleo.
Aliomba pia Watanzania wote kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja
kuulinda na kuudumisha Muungano ulioachwa na waasisi wa Taifa, hayati
Mwalimu Julius Nyerere na Shehe Karume.
chanzo:Habarileo.
Comments