
Akizungumza katika kikao maalum huko Makunduzi kilichoandaliwa na Baraza la Vijana Taifa Katibu wa Baraza la wilaya ya makunduchi Kubwa Haji Tuwani na wajumbe wake amesema ili kutimiza azma ya serikali vijana kujiajiri wenyewe hakuna budi kwa viongozi kuwawezesha vijana kwa kuwapa mitaji itayoweza kuwainua ili kubuni miradi hiyo.
Kwaupande wake kiongzi wa baraza la Vijana taifa Katibu Mtendaji na Ujumbe wake wamewataka vijana hao kuwacha tabia ya kuwatengemea viongozi wa majimbo na badala yake wabuni miradi ya maendeleo kwani Wizara ya kazi Uwezeshaji ,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto chini ya Idara ya uwezeshaji imekusudia kuwapatia mikopo vijana ili kuendeleza miradi hiyo.
Hata hivyo wametoa wito kwa vijana baada ya kuazisha miradi hiyo itaweza kuwaingizia Fedha ambazo zitasaidia kuendesha shughuli zao kufungua Akauni ili kuepusha migogoro itakayowaondolea uwaminifu kati yao.
Ziara hiyo ya siku moja iliyofanyika katika Wilaya ya kati na kusini unguja ambayo iliyakutanisha mabaraza ya wilaya zote katika mkoa wa kusini.
chanzo:Zanzibar24
Comments