
Wakizungumza na mwanahabari wetu baadhi ya mashuhuda katika tukio
hilo Hija Ali Hija na Habiba Mohamed wamesema tukio hilo limetoka jana
majira ya saa 11 jioni na jitihada za uwokozi zilifanyika lakini
alishindikana kupatikana hadi leo baada ya kikosi cha uwokozi kufika
katika tukio hilo.
Kwaupande wake Daktari wazamu wa Hospitali ya
Kivunge Makame Mdungi Makame amethibitisha kupokea mwili wa kijana huyo
aliyefariki dunia baada ya kuzama katika mto, huko kilombero na
amesema kifo chake kimesababishwa na kunywa maji mengi katika mto huo.
Aidha Daktari huyo alitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa
kuwadhibiti watoto wao kucheza karibu na mito na maeneo yaliyotuama
maji ili kuepukana na majanga yanayoweza kujitokeza.
Matukio ya kuzama kwa watoto katika kijiji cha kilombero hutokea mara kwa mara hususani kipindi kama hichi cha mvua.
chanzo:Zanzibar24.
Comments