
Shirika la kimataifa linalopambana na matumizi ya silaha za kemikali OPCW limesema linakusanya ushahidi.
Naye
mkuu wa sera za mambo ya nje ndani ya Umoja wa Ulaya, Federica
Mogherini amesema pande zote na wadau kwenye vita ya Syria wanatakiwa
kupata suluhu ya kisiasa.
Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano kuhusu mustakabali wa
Syria, Mogherini amesema EU inategemea kila mmoja kutimiza wajibu wake
kumaliza vitendo vya umwagaji damu.
''sisi Umoja wa Ulaya, si
tunaotekeleza mashambulizi, sisi si tunaopigana, sisi ndio tunaotoa
misaada ya kibinaadam, kuusaidia Umoja wa mataifa kufikia makubaliano na
suluhu ya kisiasa na sisi ndio tunaokuwa tayari kuwasaidia raia wa
Syria kujenga mustakabali wao kwa ajili ya taifa lao, hii ndio njia
tunayotumia, hii ndio namna tunavyoamini sera ya nje inavyopaswa
kutekelezwa, na tunasisitiza hilo, lakini haimaanishi kuwa mtu aharibu
kila kitu kisha tulipe gharama. hili kamwe haliwezi kutokea'' alieleza.
Kufuatia
shambulio la anga jimboni Idlib kulitolewa ripoti zikisema kuwa mamia
ya watu hasa watoto walikuwa wakitapika, kupaliwa na kutoja povu mdomoni.
Serikali
ya Marekani imesema shambulio lililotekelezwa Syria ni la kukemewa.
Msemaji wa Serikali Sean Spicer ameinyooshea kidole serikali ya Rais wa
Syria, Bashar Al Assad kuhusika na mashambulizi hayo.
Syria
imekana kutumia silaha za kemikali.Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
litakutana kwa dharura siku ya Jumatano kujadili shambulizi hilo.
chanzo:Bbc.
Comments