
Asteroidi hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na kipenyo cha karibu
kilomita moja, ilipita karibu na dunia umbali wa mara tano hivi umbali
kati ya Dunia na Mwezi.
Jiwe hilo ambalo limepewa jina 2014 JO25, ndilo kubwa zaidi kupita karibu na dunia tangu 2004.
Wataalamu wa anga za juu walisema fursa nzuri zaidi ya kutazama asteroidi hiyo angani itatokea Jumatano usiku.
Picha za mitambo ya rada zilizopigwa kwa kutumia antena ya
Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) iliyo na urefu wa 70m (230 ft)
katika kituo chake California zilionesha kwamba jiwe hilo lenye umbo la
njugu linazunguka mara moja kila baada ya saa tano.
Asteroidi hiyo iliipita Dunia katika umbali wa kilomita milioni 1.8 (maili 1.1 milioni) saa 13:24 BST mnamo Jumatano, 19 April.

chanzo:Bbc.
Comments