Idadi ya walioaga dunia kwa homa ya uti wa mgongo Nigeria ni ya kuogofya.

Wizara ya Afya ya Nigeria imesema idadi ya watu walioaga dunia kufikia sasa kutokana na homa ya uti wa mgongo imefikia 745.

Kitengo cha Kudhibiti Magonjwa cha Nigeria NCDC kimetoa taarifa kikieleza kuwa, mbali na vifo hivyo vya mamia ya watu aghalabu yao wakiwa watoto wadogo, kumeripotiwa kesi 8,057 za watu wanaoshukiwa kuugua ugonjwa huo haswa katika eneo la kaskazini mwa nchi; katika majimbo ya Zamfara, Katsina, Kebbi, Niger na Sokoto.

Habari hii ya kuendelea kusambaa kwa ugonjwa huo imeripotiwa katika hali ambayo, Alkhamisi iliyopita maafisa wa Wizara ya Afya ya Nigeria walianzisha kampeni kubwa ya utoaji chanjo katika jimbo la Zamfara kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, eneo ambalo ni kitovu cha mlipuko wa ugonjwa huo.
Kampeni hiyo ya chanjo inatazamia kuwafikia watu laki tano wenye umri wa kuanzia miaka 2 hadi 29 huku duru za kiafya zikiarifu kuwa yumkini ugonjwa huo unaoathiri ubongo na uti wa mgongo ukasambaa na kuenea katika nchi jirani ya Niger.
Itakumbukwa kuwa, homa ya uti wa mgongo au Menengitis iliua watu 33 mwaka uliopita wa 2016, huku wengine zaidi ya elfu 2 wakiaga dunia kutokana na ugonjwa huo mwaka 2009.
Aidha watu 1,100 walipoteza maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo katika nchi za Nigeria na Niger mwaka 2015, ambapo kesi zaidi ya elfu 10 ziliripotiwa.

 chanzo:parstoday.

Comments