
Rex Tillerson pia atakutana na maafisa washirika wa nchi za mashariki ya kati kabla ya kwenda Moscow.
Uingereza ilipendekeza kutolewa kwa onyo la kuweka vikwazo vikali kwa Urusi na maafisa wa jeshi la Syria.
Mwelekeo huu unafuatia mashambulizi ya hivi karibuni ya kemikali nchini Syria.
Syria
imekana kuwa ilitimiza mashambulizi hayo ya kemikali katika mji wa Khan
Sheikhoun unaoshikiliwa na waasi wiki iliyopita ambayo yaliwaua watu
watu 89.
Shirika la habari la Associated Press lilimnukuu afisa wa ngazi za
juu Marekani akisema kuwa Warusi walifahamu shambulizi hilo la kemikali
kwasababu ndege isiyokuwa na rubani ilikuwa ikizunguka hospitali moja
mjini Khan Sheikhoun huku manusuru wakitafuta usaidizi.
Masaa
chache baadaye ndege ilirusha makombora kwenye hospitali hiyo kwa kile
kinachodhaniwa kuwa jaribio la kuficha shambulizi hilo.
Kwa mujibu
wao Marekani ilisema iliharibu sehemu ya ndege iliyotumika na Urusi
katika mashambulizi ya hewani katika kambi ya wanahewa wa Shayrat
Alhamisi iliyopita huku mashambulizi zaidi yakitarajiwa.
Rais
Trump na waziri mkuu wa Uingereza May walisema kwa njia ya simu kuwa sio
mapendekezo ya Urusi kuendelea kumuunga mkono Rais Assad.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa hivi sasa amekubaliana na rais Trump kuwa Rais Assad lazima awajibike.

chanzo:Bbc.
Comments