
Juan Manuel Santos amesema serikali inakusanya $ milioni 13.9 zitakazosaidia kukabiliana an masuala ya kibinaadamu.
Wakati huo huo mazishi ya kwanza ya wahanga 262 waliouawa katika maporomoko ya Jumamosi yamefanyika.
Lakini bado jitihada za kutafuta manusura zinaendelea.
Shirika la msalaba mwekundu limeliambia shirika la habari la AFP
kwamba bado wana muda katika saa 72 za kwanza baada ya mkasa na
wanatumai kupata manusura.
Hatahivyo matumaini yanafifia miongoni mwa
wakaazi wanaotafuta jamaa zao waliosombwa katika udongo, mawe na kifusi
vinavyotokana na maporomoko hayo yalioukumba mji huo uliopo kusini
magharibi mapema Jumamosi.
Wanaosalia bado wanasubiri usaidizi wa kibinaadamu.
Rais
Santos ameahidi uwekezaji zaidi katika mji wa Mocoa zaidi ya ilivyokuwa
awali, na kumkabidhi mamlaka waziri wa ulinzi Luis Carlos Villegas
kuusimamia mji huo.
Lakini wakosoaji wa rais Santos wanasema hatua zaidi zingechukuliwa kulilinda eneo hilo kutokanana majanga kama hayo.
chanzo:Bbc.
Comments