Msanii
Agnes Waya, maarufu Masogange anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam leo wakati kesi yake ya
tuhuma za kutumia dawa za kulevya inapokuja kwa kutajwa na kuangalia
kama upelelezi umekamilika au la.
Masogange anatarajiwa kufikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri wa mahakama hiyo, ambaye ndiye anasikiliza kesi hiyo.
Mara
ya mwisho kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo hakimu huyo alimpa onyo
mshtakiwa huyo baada ya kuchelewa kufika katika chumba cha mahakama,
hatua iliyofikiwa baada ya Wakili wa Masogange, Nictogen Itege kuieleza
mahakama kuwa mteja wake yuko njiani anakuja.
Taarifa
hiyo ilisababisha, Hakimu Mashauri kumuhoji kuwa mbona yeye yupo
mahakamani? Akadai kuwa walipita njia tofauti ndiyo sababu ikatokea kuwa
mmoja kafika mwingine bado.
Hakimu
Mashauri alisema mteja wake anatakiwa afuate masharti ya dhamana na
mamlaka. Hata hivyo, baada ya muda kidogo Masogange alionekana katika
viwanja vya Mahakama wakati kesi yake tayari ilikuwa imeahirishwa.
Awali,
akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Constantine Kakula alidai
kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani
ya Jiji la Dar es Salaam Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya
Heroin (Diacety Imophine).
Katika
shtaka la pili, Kakula alidai kuwa kati ya Februari 7 na 14, 2017
mtuhumiwa huyo alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam na kwamba
alifanya makosa hayo chini ya kifungu cha 18 (a) cha Sharia ya Kupambana
na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, Masogange alikana na yuko nje kwa dhamana ya
wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh. milioni 10.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments