Afariki Dunia kwa tuhuma za wizi wa Muhogo.

Watu wasiojulikana wamemshamblia kijana Hassan Mohd Khalfan (26)  mkaazi wa hawai kwa silaha za jadi na kusababisha kifi chake.

Akisibitisha tukio hilo Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi Hassan Nassir Ali amesema kuwa tukio hilo  la kusikitisha limetokea juzi majira ya saa 10 jioni huko hawai baada ya kijana huyo kutuhumiwa kuiba muhogo katika shamba ya mtu ambae bado hajajulikana na ndipo walipo mshambalia mtu hyo kwa silaha za jadi na kupelekea kifo chake.

Aidha kamanda huyo amesema upelezi juu ya tukio hilo umeanza kufanywa na atakae bainika kuhusika na tukio la kifo cha kijana huyo  hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
chanzo:zanzibar24.

Comments