ZECO yapewa siku 14 kulipa deni.

Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) limetoa notisi ya siku 14 kwa wateja wake wote likiwamo Shirika la Umeme Zanzibar(ZECO) kulipa madeni yao.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo amesema hadi sasa deni hilo limefikia Shilingi bilioni 275 ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya shirika hilo.

Aidha amesema kuwa notisi hiyo ni kwa wateja wote wakubwa na wadogo  wasiolipa watakatiwa umeme likiwemo shirika la umeme Zanzibar.
chanzo:zanzibar24.

Comments