Mashine hizo za
ukaguzi zilizotolewa na serikali ya China,zimegharimu Sh20.2 bilioni.
Akizungumza leo
wakati wa uzinduzi wa mashine tatu za kukagulia mizigo katika makontena,
Mbarawa alisema kama wafanyakazi hawatakuwa waaminifu uwepo wa mashine hizo
hautakuwa na maana.
‘‘Leo tumezindua
mashine hizi za kisasa za kukagulia mizigo kwenye makontena lakini kama
watumishi wetu hawatakuwa waaminifu hazitatusaidia,’’alisema na kuongeza :
‘‘Mkurugenzi
Mkuu wasimamie kwa karibu watalaam watakaokuwa wanazisimamia ‘scanner’ ili
zifanye kazi iliyokusudiwa, wakikosa uaminifu waondolewe.’’ alisema.
Chanzo:Mwananchi.
Comments