Utafiti uliofanywa na shirika la lugha duniani World Linguistic
Society umesema Uganda inaongoza ikifuatiwa na Zambia halafu Afrika
Kusini ikiwa katika nafasi ya tatu na Kenya katika nafasi nne.
Kulingana na gazeti la The New Vison
nchini Uganda, utafiti huo unajiri kufuatia kanda ya video
iliomuonyesha malkia wa urembo kutoka Rwanda akishindwa kujielezea
kiingereza.
The New Vison linasema kuwa mwaka 2015, mmoja wa
malkia hao wa Urembo katika shindano la Malkia wa urembo nchini Rwanda
Uwase Honorine alishindwa kujibu maswali aliyoulizwa na majaji wa
shindano hilo.
Rwanda iliokuwa chini ya koloni ya Ufaransa ilianza kuzungumza Kiingereza baada ya kukosana na Ufaransa.
Gazeti
la The New Vision linasema kuwa kiingereza nchini Uganda ndio lugha
rasmi, na ndio lugha inayotumiwa katika shule na taasisi tofauti nchini
humo.
Watoto huanza kujifunza lugha hiyo katika shule za msingi.
The
New Vison linasema kuwa hivi majuzi serikali iliziagiza shule kufunza
lugha za nyumbani kwa wale wanaosoma katika shule za msingi lakini
ikasisitizia kuwa Kiingereza ndio lugha itakayotumiwa katika mtaala.
Mataifa yanayozungumza kiingereza kwa ufasaha:
1.Uganda
2. Zambia
3. South Africa
4 . Kenya
5. Zimbabwe
6. Malawi
7. Ghana
8. Botswana
9. Sudan
chanzo:Bbc.
Comments