Dk Mgwatu amesema kukamilika kwa boti hizo ni utekelezaji wa ahadi za
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa
alizozitoa kwa wananchi wa Pangani mkoani Tanga pamoja na Kilambo na
Msangamkuu mkoani Mtwara kwa nyakati tofauti.
Aliongeza kuwa boti hizo nne zitatoa huduma za dharura hasa wakati wa
usiku kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa na pia kutoa usafiri mbadala
wakati vivuko vikubwa vinapokuwa haviwezi kutoa huduma kutokana na
changamoto mbalimbali ikiwemo kupungua kwa kina cha maji katika maeneo
ya Kilambo pamoja na Utete mkoani Pwani.
Naye Mkurugenzi kutoka Kampuni ya Songoro Marine Boatyard, Major
Songoro alisema boti tatu kati ya nne zilizokabidhiwa zimejengwa kwa
kutumia ‘fibre glass’ na boti moja imejengwa kwa kutumia chuma.
Boti ya Mv Kuchele ambayo itapelekwa katika eneo la Msangamkuu Mtwara
ina uwezo wa kubeba abiria nane, sawa na boti ya MV Bweni
itakayopelekwa Pangani mkoani Tanga.
Mv Mkongo itakayopelekwa Utete, ina uwezo wa kubeba abiria 40 na MV.
Tangazo itakayopelekwa Kilambo/Namoto Mtwara ina uwezo wa kubeba abiria
25.
Aidha, Dk Mgwatu aliishukuru serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano kwa kuwezesha ujenzi wa boti hizo na tayari
amemuagiza mkandarasi huyo kuhakikisha anazisafirisha boti hizo kwenye
maeneo husika haraka iwezekanavyo ili wanachi waanze kunufaika na huduma
mbadala itakayotolewa na boti hizo.
Ujenzi wa boti hizo umefanywa kwa kutumia fedha za ndani na umegharimu jumla ya Sh milioni 415.
chanzo:Habarileo.
Comments