Akizungumzia mfumo huo Ofisa wa
SSRA David Nghambi alisema mfumo huo mpya utaiwezesha SSRA kupokea na
kushughulikia malalamiko hayo moja kwa moja kwa wakati.
Alisema mfumo huo unaotambuliwa
kwa jina la SSRA upo kwa njia ya mifumo ya simu (mobile application)na
unapatikana kwa njia ya simu za mkononi kupitia mtandao wa google hivyo
mtu yeyote anaweza kuupakua na kuweka malalamiko yake.
"Mfumo huu hauna hatua
nyingi kwani unakuingiza moja kwa moja katika ukurasa utakaokuwezesha kuingiza
malalamiko yako na mamlaka itaweza kuyashughulikia" alisema
chanzo:Mwananchi.
Comments