Serikali: wananchi watakiwa kufuata sheria kumiliki mashamba ya mikarafuuu Pemba.

serikaliSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema hakuna mtu yoyote alinyang’anywa shamba la mikarafuu huko pemba bali wananchi wanatakiwa kufuata utaratibu wa kisheria (mikataba) ili waweze kupatiwa umiliki halali wa mashamba hayo.
Akijibu swali katika kikao cha Baraza la wawakilishi huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar kuhusu kurejeshwa kwa mashamba ya wananchi,
Naibu waziri wa Kilimo, mifugo, Maliasili na Uvuvi Zanzibar Lulu Mshamu Abdallah amesema mashamba hayo yapo katika mikono ya Serikali kutokana na kuachwa na wananchi kwa muda mrefu bila kufanyiwa shughuli za kilimo.
Aidha amesema Serikali inaendelea na utaratibu wa kuyatafuta mashamba hayo ili kuwaruhusu wananchi wenye mikataba halali waweze kuendelea na shughuli zao katika utaratibu wa kisheria uliowekwa.
Hata hivyo ametowa wito kwa wananchi kuendelea na upandaji wa miti mbalimbali ikiwemo miti ya mikarafuu  katika mashamba hayo ya eka tatu na mashamba yao ya Urithi ili wananchi waweze kujipatia kipato cha kuweza kujikimu kimaisha.
chanzo:zanzibar24.

Comments