RITA yakana kuidhinisha mabadiliko wadhamini CUF.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy HudsonWAKALA wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) imesema hakuna mabadiliko yoyote yaliyoidhinishwa kwenye Bodi ya Wadhamini wa Chama cha Wananchi (CUF).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Emmy Hudson, RITA haijafanya mabadiliko yoyote na kuwa kwa sasa inafanyia kazi maombi yaliyowasilishwa na chama hicho ya mabadiliko wa Bodi ya Wadhamini.


“RITA inaufahamisha umma kwamba hakuna mabadiliko yoyote yaliyoidhinishwa kuhusu Bodi ya Wadhamini ya CUF na maombi yaliyowasilishwa bado yanafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu zinavyoelekeza,” alisema Hudson ambaye pia ni Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu.
 chanzo:Habarileo.

Comments