Yeye na mama yake wanadaiwa kulaghaiwa kuingia ndani ya teksi ya basi
dogo kabla ya kufanyiwa maasi hayo na kuamrishwa kukabishi kadi yake ya
benki pamoja na namba za siri(PIN) za kadi ya benki Pna wanaume watatu
waliokuwa wamejihami kwa bunduki.
Inadhaniwa kuwa kuwa hili lilikuwa ni shambulio la hivi karibuni la genge la majambazi.
Taarifa za kwanza za "teksi za ubakaji " zilitolewa mwaka mmoja uliopita.
kwa
mujibu wa rekodi za Roodeport, mashambulio ya awali ya ubakaji
yaliripotiwa mwezi Machi 2016, huku mashambulio matatu yakifanyika
katika kipindi cha wiki ya mwisho ya mwezi Juni.
Matukio yote yalifanyika ndani ama karibu na kitongoji cha Soweto mjini Johannesburg.
hata
hivyo haijjabainika wazi ni mashambulio mangapi yaliyokwisha tokea huko
katika kipindi cha miezi 12, ama ikiwa yote yalitekelezwa na genge hilo
hilo.
Luteni kanali Lungelo Dlamini ameiambia BBC: "Kikundi cha
wanaume watatu ama wawili waliokuwa wakiendesha magari mawili tofauti ya
[Toyota] Quantums, moja la rangi ya majivu na jingine la rangi
nyeupe, yali wachukua wanawake wawili yakijifanya ni magari ya teksi,
wakawapora kwa silaha na baadae kuwabaka."
Bwana Dlamini
amesema kuwa haijabainika wazi kuwa magari hayo ya Quantum yalikuwa yana
njama moja ama kila moja lilikuwa linatekeleza uhalifu huo kivyake.
Hadi
sasa, wanawake wawili -akiwemo mama wa mvulana huyo -wamekwisha
zungumza na vyombo vya habari vya Afrika Kusini, kuelezea kilicho
wasibu.
Mwanamke wa pili alikiambia kituo cha redio cha Kaya FM
namna mwanamume aliyempata baada ya kushambuliwa aliwasaidia wanawake
wengine wanaodhaniwa kubakwa katika eneo hilo hilo .
Amesema genge hilo limekuwa likiendesha uhalifu huo, kulingana mtandao wa habari wa -Afrika News network.
Wanawake wote wawili walichukuliwa nyakati za mchana.
Baada
ya mama na mwanae kuingia ndani ya teksi, mvulana alilazimishwa kulala
kifudi fudi chini kwenye sakafu ya gari hilo, huku wanaume watatu
wakimbaka mama yake.
Muathiriwa huyo aliliambia shirika la habari
la EyeWitness News kwamba alikuwa anaomba wakati wa tukio hilo majangili
wasimuumize mwanae.
Afrika Kusini ina viwango vya juu vya visa vya ubakaji vinavyoripotiwa duniani.
chanzo:Bbc.
Comments