Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru alisema hayo na
kuongeza kuwa, ili kukabiliana na changamoto hiyo, wameanza ukarabati
katika majengo yao manne hospitalini hapo likiwemo la akina mama, jengo
kuu la upasuaji, watoto na tiba ya meno.
Profesa Museru alisema hospitali hiyo ina vyumba vya upasuaji 13
ambavyo havikidhi mahitaji halisi na utoaji wa huduma bora na za haraka
kwa wagonjwa.
Alisema kutokana na upungufu huo, wagonjwa wamekuwa wakisubiri kwa
muda mrefu ili kupata huduma ya upasuaji, hivyo Muhimbili imeanza
ukarabati wa jengo la upasuaji wa akinamama kutoka vyumba viwili hadi
vinne, jengo kuu la upasuaji kutoka vyumba saba hadi nane, jengo la
watoto kutoka vyumba viwili hadi vinne na jengo la tiba ya meno kuwa na
vyumba viwili.
“Ukarabati huu utasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa wanaosubiri
upasuaji ambapo wengine wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu wakati
mwingine kufikia hata mwaka.
Baada ya ukarabati huu kukamilika,
hospitali itaongeza vyumba vya upasuaji saba na kufanya iwe na jumla ya
vyumba ishirini,” alisema.
chanzo:Habarileo.
Comments