
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake Mwanakwerekwe,
Mkuu wa kitengo cha bei Ofisi ya Mtakwimu mkuu wa Serikali, Khamis
Ahmada Shauri, alisema, kasi hiyo imechangiwa na kuongezeka bei kwa
bidhaa za vyakula na zisizokuwa za vyakula.
Alisema, bei za vyakula na zisizokuwa za vyakula zimeongezeka kwa
asilimia 4.4 kwa mwezi februari kutoka asilimia 3.5 ya mwezi januari.
Aidha kwa upande wa farisi za bei, ziliongezeka kwa 100.2 mwezi februari ikilinganishwa na 95.6 mwezi januari.
Akizungumzia mfumuko huo, alisema mfumuko huu umekuwepo kwa karibu
kipindi cha miezi minne huku akisistiza kuwa hali hiyo inachangiwa na
kasi ya bei katika masoko ya bidhaa na nishati.
Nae Meneja Msaidizi Idara ya Uchumi ya Benki Kuu tawi la Zanzibar,
Moto Ng’winganele Lugobi, alisema pamoja na mfumuko huo kuongezeka, bado
Zanzibar imefikia hatua nzuri kulinganisha na malengo yaliyowekwa ya
asilimia 8 kwa nchi za Afrika Mashariki.
“Tunasema ni hali nzuri kwasababu bado tupo bado tupo kwenye tarakimu moja, si hali ya kutisha” alisisitiza.
Alisema Mfumuko wa bei upo kwa karibu nchi zote za Afrika Mashariki
ikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania Bara na Rwanda. Mfumuko wa bei Tanzania
bara umeongezeka kutoka 5.2 mwezi januari hadi kufikia 5.5 mwezi
februari, ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.3 kiasi ambacho hakina
athari katika uchumi wa nchi.
chanzo:zanzibar24.
Comments