Amesema itakua ni jambo la busara kwa Maofisa hao kuutumia muda wao wa kazi wakiwa maofisini na huku akiwataka kubadilika ili kwenda sambamba na kazi ya utendaji wa Serekali kuu.
Akizungumza na Maofisa wa Idara na Taasisi za Serekali Katibu Tawala wilaya hiyo Mussa Ali Moh’d kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amesema kila mmoja anatakiwa kuwajibika kutekeleza wajibu na majukumu yao ya kazi.
Aidha amewataka kuwasilisha taarifa za ofisi zao kwa wakati pamoja na kuzitoa ili wananchi waweze kutambua maendeleo yanayofanywa na serekali yao.
Akizungumza katika kikao hicho Afisa Ustawi wa jamii Haroub Sleiman Hemed amewaomba maafisa hao kushirikiana kudhibiti matendo ya udhalilishaji.
Kikao hicho kimeandaliwa na Serekali ya Wilaya hiyo ili kujadili changamoto zinazojitokeza pamoja na kutafuta ufumbuzi wake .
chanzo:zanzibar24.
Comments