Kamanda wa
polisi mkoani hapa, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kwamba Msalia alifariki jana saa 5.00 usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
wa Dodoma.
Amesema marehemu
aliondoka nyumbani kwake kwa kutumia gari aina ya Prado na kwenda kujipiga
risasi katika eneo la Veyula nje kidogo ya mji wa Dodoma.
"Tulipata
taarifa ya kujipiga risasi jana saa 3.00 na polisi walipokwenda waliokota
maganda matano katika eneo la tukio na walipompeleka hospitali hawakuweza
kuokoa maisha yake kwa sababu alikuwa amejichana chana na risasi, "amesema.
Alipoulizwa kama
kifo hicho kunatokana na sakata la ukamataji wa viroba, Mambosasa amesema
anafikiri suala hilo ni hisia tu kwasababu marehemu alikamatwa Machi 3 mwaka
huu akiwa na shehena ya tani 1.5 za pombe ya viroba.
chanzo:Mwananchi.
Comments