Mirosalva Breach alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake nje ya makazi yake mjini Chihuahua.
Mmoja wa watoto wake ambaye alikuwa naye ndani ya gari, hakujeruhiwa.
Watu wenye silaha waliacha ujumbe uliosema '' kwa kuwa na mdomo mrefu''.
Bi
Breach aliripoti kuhusu masuala ya uhalifu, biashara ya dawa za kulevya
na rushwa katika gazeti la kitaifa, mjini humo La Jordana na Notre de
Juarez.
Kamati inayotetea waandishi wa Habari imesema wanahabari 38 wameuawa nchini Mexico tangu 1992.
chanzo:Bbc.
Comments