Mama
mlezi wa aliyekuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Kikwete, Bi Nuru binti Halfani Shomvi amefariki dunia katika Hospitali
ya Muhimbili alipokuwa akitibiwa asubuhi ya leo.
Kupitia
mtandao wa twitter, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akishukuru jamii kwa
salamu za pole alizopokea amesema shughuli za msiba ziko nyumbani kwa
marehemu Mzee Kikwete, Mtaa wa Caravan, Bagamoyo na maziko yatakuwa
Bagamoyo mjini, kesho Jumatano Machi 8, 2017 saa 10 Alasiri.
"Mama
amefariki jana usiku saa nane, akiwa na miaka 91. Baba yangu, Mzee
Halfani Mrisho Kikwete alikuwa na wake wawili alipofariki 1998. Mama
yangu mzazi Bi Asha binti Jakaya, aliyekuwa mke mkubwa wa Mzee Halfani
Kikwete alifariki 1999; tukabaki na mama yetu huyu mdogo". Kauli ya
Jakaya Kikwete.
Naye
Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ambaye ni mjukuu wa marehemu
ndiye aliyekuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa kifo hicho asubuhi ya
leo.
"Ndugu
na marafiki nasikitika kuwatangazia msiba/kifo cha Bibi yetu Bi. Nuru
Khalfan Kikwete kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili
alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana" Amesema Ridhiwan Kikwete.
Ndugu wapendwa, nawashukuru sana kwa salamu za pole na upendo kufuatia
kifo cha Mama yangu mdogo mpendwa Bi Nuru binti Halfani Shomvi. – JK
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7,
— Jakaya Kikwete (@jmkikwete) March 7,
Chanzo:Mpekuziblog.
Comments