Washitakiwa hao ni Sultan Ibrahim (36) mkazi wa Usalama Temeke,
Augustino Kalumba (39) raia wa Zambia walifikishwa mahakamani hapo na
kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Aidha, mshitakiwa Ibrahim alipandishwa tena kizimbani na Ramadhan
Hamisi (48) ambaye pia ni dalali mbele ya Hakimu Mkazi, Respicious
Mwijage.
Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga alidai mbele ya Hakimu
Simba kuwa washitakiwa Ibrahim na Kalumba wanakabiliwa na mashitaka
matatu ya uhujumu uchumi.
Katuga alidai kuwa washitakiwa wote kwa pamoja kati ya Desemba Mosi
mwaka jana na Machi Mosi mwaka huu, maeneo yasiyofahamika walikula njama
kinyume na kifungu namba 193 cha Sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
ya Kudhibiti Ushuru ya Mwaka 2004. Alidai washitakiwa hao walikula njama
kusafirisha mali iliyofichwa kinyume na sheria hiyo.
Katika mashitaka ya pili ilidaiwa kati ya Desemba mosi na 31 mwaka
jana, maeneo ya Mamlaka ya Usimamizi Bandari Tanzania (TPA), waliingiza
magari matatu aina ya Range Rover Sports yenye chesisi namba SALW 2KE
9EA 388884 ya rangi nyeusi, chesisi namba SALVA 2CE 4EH 948974 nyeupe na
SALGA 2JEODA 115580 yakiwa yamechanganywa na mitumba ya viatu, mabegi
na nguo kwenye kontena namba MSKU 9914162.
Pia inadaiwa kati ya Desemba mosi mwaka jana na Machi mosi mwaka huu
maeneo ya Bandari wilayani Temeke washitakiwa hao waliingiza mali
iliyofichwa na kusababisha serikali kukosa mapato ya Sh milioni 287.8.
Pia Ibrahim na Hamisi walipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo
mbele ya Hakimu Mwijage ambapo walidaiwa kusababisha hasara ya Sh
milioni 190.9.
Katuga akishirikiana na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi alidai
washitakiwa hao walikula njama kutenda kosa hilo kinyume na sheria ya
ushuru kwa kuingiza mali iliyofichwa.
chanzo:Habarileo.
Comments