Chama
Cha Mapinduzi (CCM) leo kinafanya vikao viwili vikubwa kwa mkupuo vya
Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma.
Vikao
hivyo vitafanyika kwa siku moja, baada ya Kamati Kuu kutofanyika jana.
Badala yake siku nzima ya jana, ilitumika kwa ajili ya kikao cha Kamati
ya Usalama na Maadili ya chama.
Kikao
hicho cha Kamati ya Usalama na Maadili cha jana, kiliangalia maadili ya
wanachama wake na kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais John
Magufuli.
Pamoja
na mambo mengine, kikao hicho hujadili nidhamu za viongozi na baadhi ya
wanachama waliokwenda kinyume na maadili ya chama hicho.
Kamati hiyo huhoji wanachama na viongozi na mapendekezo yake, hupelekekwa Kamati Kuu kwa ajili ya hatua zaidi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini hapa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,
Humphrey Polepole alisema, vikao hivyo vitafanyika leo, ambapo Kamati
Kuu itakutana asubuhi.
Alisema
baada ya Kamati Kuu kumaliza kikao chake, mchana Halmashauri Kuu
itafanya mkutano wake, ambao ndio utakaoandaa ajenda kwa ajili ya
Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho, utakaofanyika kesho, ambao utafanya
mageuzi makubwa katika chama.
Baadhi
ya mageuzi hayo ni kubadilisha Katiba na Kanuni za chama pamoja na
jumuiya zake, ikiwemo kupunguza wajumbe wake ili kuwa chama cha ufanisi
zaidi.
Polepole
aliwaomba wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa yote nchini, kuwasili
mjini Dodoma na kuhudhuria kutokana na maandalizi yake kukamilika.
“Nawaomba
wajumbe wa Mkutano Mkuu wafike mjini Dodoma kutokana na maandalizi yote
kukamilika ili kufanikisha mkutano huo ambao ni muhimu katika kufanya
mageuzi katika chama,” alisema Polepole.
chanzo:mpekuziblog.
Comments