Lipumba amkaimisha Sakaya nafasi ya Maalim Seif.

sakayaBaraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama cha Wananchi(CUF) leo limemvua Maalim Seif nafasi ya Ukatibu Mkuu na kumpa Magdalena Sakaya.

Taarifa hiyo imetangazwa mapema leo na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) ambae anatambulika na baraza la wasajili wa vyama vya siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba, na kumteu mh sakaya kutokana na kazi yake nzuri anayo ifanya katika chama.


Sababu ya kukaimishwa sakaya katika nafasi hiyo ni kutokana na Maalim Seifu kutofika ofisini nakuto hudhuria  kwa baadhi ya vikao vinavyo endeshwa na CUF vinavyo tambuliwa kikatiba na chama hicho.

Chanzo: zanzibar24.

Comments