Jeshi la Korea kusini limesema Korea kaskazini imerusha makombora yake
kadhaa katika bahari ya Japan, Jeshi la Korea kusini limesema kuwa
makombora hayo yamerushwa kutoka kwenye eneo la Tongchang-ri lililo
kwenye mpaka kati ya Korea kaskazini na China na kurushwa kwa umbali
takriban kilomita elfu moja.
Akiongea na waandishi wa habari, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe
amesema makombora hayo yanadhihirisha ushaidi tosha wa vitisho vipya
kutoka kwa Korea kaskazini.
''Korea kaskazini imefyatua makombora
yake manne leo na kuangukia karibu na eneo letu la maji lenye manufaa
kwetu kiuchumi.Japan itakusanya taarifa na kuzichambua kuhusu tukio
hili.Japan inaipinga vikali .
Korea kaskazini.makombora yaliyorushwa
wakati huu inaonyesha wazi kuwa Korea kaskazini ni tishio jipya.Korea
kaskazini ilishatangaza aina hii mpya ya makombora kabla ya kuyarusha
leo hivyo, tutafuatilia kwa karibu suala hili kwa kwa umakini mkubwa''
chanzo:Bbc.
Comments