
Akizungumza na Waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai Zanzibar Ramadhani Ng`anzi amesema ukatwaji huo umekuja
baada ya upelelezi uliofanywa na jeshi la polisi kwa makundi matatu ya
watu wakiwemo wafanyabiashara na kubahatika kuwakamata wasambazaji hao.
Hata hivyo amesema katika operesheni hiyo pia madawa ya aina
mbalimbali yamekamatwa ikiwemo Heroin na Cocain Grams 3450.32,madawa
mengine ni ya vidonge valium 493, Bhangi 203 na Mirungi kg46 pamoja na
gari moja na pikipiki tatu ambazo zilikuwa zinatumika kusambazia
biashara hiyo.
Aidha amesema opereshen hiyo imeleta faida kubwa kwa jamii na jeshi
la Polisi kutokana na kupungua kwa vigenge vya madawa ya kulevya na
kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili wahusika waweze
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Jumla ya shilingi millioni nne laki tatu na ishirini elfu zimekamatwa
katika operesheni hiyo na kesi 87 zimefunguliwa tangu kuanza kwa
operesheni hiyo february mwaka huu.
chanzo:Zanzibar24.
Comments