Robin Camp alijiuzulu baada ya kamati ya nidhamu kupendekeza kuwa afutwe kazi.
Bwana
Camp alisema kuwa alisikitishwa na matamshi yake lakini jopo la nidhamu
lilisema liliona matamshi yake yalikosa hali ya kutopendelea na
heshima.
Waziri wa haki katika jimbo hilo amekubalia kujiuzulu kwake.
Matamshi
ya bwana Camp yaliotolewa wakati wa keshi ya ubakaji mwaka 2014 yalizua
hisia kali na kusababisha ukosoaji mkali kutoka kwa waathiriwa wa
unyanyasaji wa kingono pamoja na mawakili wao.Jaji huyo alichukua
msimamo na kuliambia baraza hilo kwamba alifahamishwa kuhusu makosa yake
na kwamba aliomba msamaha juu ya matamshi yake.
Baraza hilo ambalo husimamia idara ya haki lilibaini kwamba vitendo
vya bwana Camp wakati wa keshi hiyo vilikuwa na uharibifu wa wazi kuhusu
sera ya kutoa haki katika idara hiyo na kwamba hawezi kuendesha tena
afisi hiyo.
Pia ilibainika kwamba jaji huyo alizungumza na mlalamishi kwa lugha isioheshimika inayofedhehesha na kuonyesha ubabe.
chanzo:bbc.
Comments