Bwana Trump amemwalika Abbas baada ya mazungumzo ya kwanza ya simu na kiongozi huyo tangu aingie maamlakani.
Trump
amependekeza kuhusika katika juhudi za amani mashariki ya kati, japo
viongozi wa Palestina wanalalamika kwamba sera ya kigeni ya rais Trump
inaonekana kupendelea Israeli.
Hakujakuwa na mazungumzo ya amani
ya haja kati ya Israel na Palestina tangu mazungumzo ya amani
yalioanzishwa na Marekani kugonga mwamba mnamo mwezi Aprili 2014.
Msemaji
wa Trump Sean Spicer alithibitisha siku ya Ijumaa kwamba rais wa
Marekani alimualika Abbas katika ikulu ya Whitehouse hivi karibuni.
Rais huyo alimwambia kiongozi huyo wa Palestina kwamba watajadiliana
vile watakavyoanzisha tena mazungumzo ya amani kulingana na msemaji wa
Abbas aliyenukuliwa na Reuters akisema.
Alisema kwamba bwana Trump
alisisitiza kuhusu juhudi zake za mpango wa amani ambao utaleta amani
ya kweli kati ya Palestina na Israel.
chanzo:Bbc.
Comments