
Akizungumza na kituo cha redio cha Clouds Fm, Bimani amesema mkutano
halali unaotambulika ulifanyika Machi, 19 na maamuzi yote yalifanywa
kwemye kikao hicho hivyo maamuzi yanayotolewa sasa hayana uhalali.
Aidha msemaji huyo amewataka wanachama wa CUF kutokuwa na hofu na
kupuuzia maamuzi yaliyotolewa na Prof. Lipumba na kuwa Maalim Seif
atasalia kuwa Katibu Mkuu wa chama kama jinsi ilivyokuwa awali kabla ya
kutangazwa kuvuliwa Ukatibu Mkuu.
“Tunapenda kuwambia wanachama wa CUF mkutano walioufanya
haukubaliki na hakuna kikao halali kilichofanyika na hata washiriki wake
hawakuwa halali … mkutano ulishafanyika na kila kitu kilifanyiwa
maamuzi hapo,” amesema Bimani.
chanzo: zanzibar24.
Comments