
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katibu Mtendaji wa baraza hilo Kajubi Mukajanga amesema kitendo cha kuvamia chombo cha habari na silaha ni kitendo cha kushtua na kutia hofu waandishi kwani ni kinyume na sheria.
Hata hivyo Kajubi amewataka viongozi wa umma kuyatumia vyema madaraka yao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao na sio kutumia mabavu kwani kufanya hivo ni kuivunja katiba na kumnyima haki mwandishi katika majukumu ya kazi zake.
Aidha ameviomba vyombo vya sheria pamoja na Mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria kutokana na tukio hilo kwani si mara ya kwanza kwa waandishi wa habari kutishiwa maisha katika kazi zao za uwandishi.
Mapema alitoa wito kwa waandishi kuwa na umoja na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kuzingatia maadili ya kazi zao katika uandikaji na utangazaji wa habari ikiwemo kuepuka kurusha au kuandika habari zisizo na tafiti wa kutosha (balance) ili kuepusha migogoro.
chanzo:Zanzibar24
Comments