Adhabu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo,
Hassan Momba baada ya mzee huyo kukiri kosa hilo aliposomewa mashitaka
yake yanayoangukia kwenye Sheria ya Dawa za Kulevya Namba 5/2015,
Kifungu cha 15 (1) (2).
Akitoa adhabu hiyo ambayo si mara ya kwanza kutolewa na mahakama
hiyo, Hakimu Momba alisema kukiri kwa mshitakiwa kunaonesha jinsi
hajutii hivyo ili iwe fundisho kwa wengine, anastahili adhabu kali.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi, Philbert
Pimma uliiambia Mahakama hiyo kwamba Machi 5, mwaka huu katika Kijiji
cha Igagala, mshitakiwa alikutwa na kilo 150 za dawa za kulevya aina ya
bangi zenye thamani ya Sh 8,351,250.
Katika kesi nyingine, Hakimu Momba amemhukumu kwenda jela miaka
mitatu au kulipa faini ya Sh milioni moja Hadija Maganga baada ya kumtia
hatiani kwa kosa la kukutwa akiwa amepanda dawa za kulevya aina ya
bangi shambani kwake.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Mkaguzi wa Polisi, Philbert Pimma
aliiambia mahakama hiyo kuwa Machi 5, mwaka huu katika Kijiji cha
Igagala, mshitakiwa alikutwa na miche 3,000 ya bangi shambani kwake
ikiwa na thamani ya Sh milioni 4.5.
Baada ya kusomewa shitaka hilo, mshitakiwa alikiri kosa hilo ndipo
Mahakama kwa kumuona na hatia ikamhukumu kwenda jela miaka mitatu.
chanzo:Habarielo.
Comments