174 washikiliwa kwa kamari, dawa za kulevya.

Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watuhumiwa 174 kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo kupatikana na dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, utapeli, wizi kutoka maungoni na kucheza kamari.

Aidha, watu hao wanatuhumiwa kuuza pombe haramu ya gongo, kupatikana na bangi na walikamatwa katika operesheni inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi wa Kanda hiyo, Lucas Mkondya alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika operesheni iliyofanyika kuanzia Machi 22 hadi 28, mwaka huu.

Alisema katika operesheni hiyo walikamata kete 75 za dawa za kulevya, puli 28, kete 542 na misokoto 103 ya bangi pamoja nalita 93 za pombe haramu ya gongo.

Aidha, Mkondya alisema watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamejeruhiwa wakati wakirushiana risasi na askari polisi katika eneo la Magengeni Chamazi.
 chanzo:Habarileo.

Comments