Watendaji wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makamanda kisiwani Pemba watakiwa kutoa ushirikiano juu ya matuzi mabaya ya mchanga.

 Na Asha Salum _ Pemba.
Image result for hamad rashid mohamedWAZIRI wa Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi , Mh. Hamad Rashid Mohammed, amewataka watendaji wa Mikoa na Wilaya pamoja na Makamanda kutoa ushirikiano wa pamoja kupiga vita matumizi mabaya ya Mazingira ,ili kupunguza kasi ya matumizi ya Rasilimali ya Mchanga kwa kuinusuru Zanzibar.
Mh. Waziri ameyasema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya hali halisi ya Rasilimali ya Mchanga, huko katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo, Weni,  Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Mh.Hamadi amesema kuwa, Serikali imeagiza kwa hatua ya kwanza kupunguza matumizi ya Rasilimali ya mchanaga kwa kutumia utaratibu nzuri unaokubalika kisheria pamoja na kutozwa faini kwa wanaokiuka taratibu hizo.
Amesema kwa kuwa Ardhi ni mali ya Serikali lazima mapato yaonekane kupitia utaratibu wa tozo zilizowekwa kupitia leseni na vibali vya uchimbaji wa rasilimali hiyo.
Kwa hatua ya pili Mh.Hamadi amesema kuwa, taaluma  inahitajika kupitia ngazi mbali mbali, ili kuwaelewesha wananchi umuhimu wa kuwepo rasilimali ya Mchanga, matumizi pamoja na maeneo yalioathirika kutokana na matumizi mabaya yaliopo nchini.
Mkutano huo wa siku moja ambao ulilenga mkakati madhubuti wa kupunguza kasi ya matumizi ya Mchanaga uliwashirikisha Makamanda wa Jeshai la Polisi wa Mikoa, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, pamoja na maafisa mbali katika Idara zinzzohusika na Mazingira Unguja na Pemba.

Comments