WADAU mbali mbali wa Sekta ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Kisiwani Pemba wapendekeza juu ya merekebisho ya sera.

Image result for Pemba,Na Asha Salum - Pemba.
WADAU  mbali mbali wa Sekta ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Kisiwani Pemba, wametoa mapendekezo ya marekebisho ya Sera ya mwaka 2012 inayotegemewa kufayakazi kwa kutoa miongozo inayokwenda sambamba na shughuli za kilimo.
Mapendekezo hayo wameyatoa katika mkutano wa mapitio ya Sera Kilimo, uliofanyika Weni, Wilaya ya Wete Pemba.
Awali akifungua mkutano kwa niaba ya Ofisa Mdhamin, Mkuu wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti Pemba, CHUM HAMAD YUSSUF, amesema marekebisho ya sera hiyo ni kwenda sambamba na mkakati wa malengo ya mkuza iii kwa kuondoa kasoro zilizopo.
Mkuu huyo wa Idara alisema kuwa, ni jambo la busara  kwa wadau hao kutoa kasoro na  mapendekezo wanayoona ni muhimu na yamekosekana katika sera hiyo,
ili kufikia malengo yaliokusudiwa kwa faida ya taifa.
Akiwasilisha sera ya marekebisho, Afisa Mipango, kutoka Idara ya Mipango Zanzibar, ALI BASHA, amesema kuwa, marekebisho ya sera hiyo, kwa kiasi kikubwa itasaidia kuondoa matatizo mbali mbali ya sekta hiyo kiutendaji na kuleta ufanisi wenye tija kwa wakulima.
Mbali na hayo, amesema kuwa, sera mpya inayofanyiwa mapitio itakuwa na maeneo 23 ambayo yatatilia mkazo katika maeneo ya kilimo, hasa katika mazao ya mizizi, matunda na mboga mboga.
Akitoa mapendekezo katika kuchangia sera hiyo Afisa Kilimo, kutoka Idara ya kilimo Pemba, JUMA MAALIM FAKI, amesema kuwa, ni vyema sera hiyo ikazingatia vyema mbegu bora zinazokwenda sambamba na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Comments