Wabunge hao ambao wote ni kutoka chama cha upinzani cha
FDC, wanasema kuwa ni kama ambaye mkubwa wao yuko katika kizuizi cha
nyumbani.
Kulingana na mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango
wabunge wanne kutoka Kasese, Winfred Kiiza, Harlod Muhindi, William
Nzoghu na Robert Muhindo wamelalamika kuwa mfalme wao anadhalilishwa.
Mfalme Mumbere amekuwa korokoroni tangu mwaka jana kwa sababu zinazohusika na uchochezi.
Serikali ilimfungulia mashtaka kadhaa ikiwemo ya mauaji, wizi na
ugaidi baada ya kumkamata kufuatia makabiliano ya risasi kati ya
maafisa wa usalama dhidi ya walinzi wa mfalme ambao serikali ilidai
walikuwa wanajihusisha na visa visivyo sawa.
Febuari 6 mwaka huu
mahakama ya juu ya mjini Jinja ilimuachilia Mumbere kwa dhamana ya
polisi ya shilling za Uganda millioni 100 sawa na dola za Marekani
27,894, na wabunge hao ndio wadhamini wake.
Pia mfalme huyo aliamriwa kuwa kila baada ya muda fulani itambidi kurudi mahakamani.
Jumatatu anatakiwa kufanya hivyo na sasa yuko nyumbani kwake hapa mjini Kampala.
chanzo:Bbc.
Comments